Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetoa jumla ya TZS 5,829,403,959 katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024 hadi Januari 2025/2026 kwa ajili ya kuwezesha timu za taifa na wanamichezo kushiriki mashindano mbalimbali.
Katibu Mtendaji wa BMT, Bi. Neema Msitha, amebainisha kuwa uwekezaji huo umesaidia kugharamia mahitaji ya timu mbalimbali, ikiwemo TZS 1,215,662,139 zilizokwisha tumika kufikia Januari ya msimu wa 2025/2026 ili kutekeleza azma ya Serikali ya kuinua sekta ya michezo nchini.
Miongoni mwa timu zilizonufaika na ufadhili huo ni Taifa Stars iliyoshiriki mashindano ya CHAN nchini Tanzania, Kenya, na Uganda Agosti 2025, pamoja na timu ya wanawake ya Twiga Stars iliyoshiriki WAFCON nchini Morocco Julai 2025.
Aidha, fedha hizo zimewezesha ushiriki wa timu za taifa za Netiboli, Pooltable, Ngumi, na timu ya watu wenye ulemavu (Amputee Football) iliyoshiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi mnamo Septemba 2025.
Chanzo; Itv