Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Diarra Aondoka na Rekodi Yake Afcon

Hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) imeacha kumbukumbu nyingi, lakini jina Djigui Diarra wa Mali ni moja ya makipa walioacha rekodi katika mashindano hayo.

Katika michezo minne ya robo fainali iliyoshuhudia jumla ya mabao 10 yakifungwa, Diarra alionyesha kiwango bora kwa kuokoa michomo ya hatari mara 7, idadi kubwa kuliko kipa yeyote aliyeshiriki hatua hiyo.

Mbali na Diarra, mchezaji wa Misri, Emam Ashour ameibuka kuwa kinara wa pasi za mwisho, akichangia mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Ivory Coast.

Mali iliondoshwa robo fainali ya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Senegal.

Mshambuliaji wa Morocco, Brahim Diaz ndiye kinara wa mabao katika fainali za AFCON 2025 akiwa amefunga 5 akifuatiwa na Victor Osimhen wa Nigeria, ambao timu zao zitamenyana nusu fainali Jumatano hii kuanzia saa 5 usiku.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: