Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Christian Ronaldo Aonywa Saudi Pro League

Mshambuliaji na nahodha wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo, amepewa onyo na bodi ya Ligi ya Saudia Arabia (Saudi Pro League) akitakiwa kufahamu kuwa hakuna upendeleo wowote unaofanywa dhidi ya vilabu vya ligi hiyo na kuiacha kando klabu yake.

Taarifa ya Saudi Pro League imeeleza: “Hakuna mtu binafsi, au staa anayefanya uamuzi nje ya klabu yake.”

“Saudi Pro League imejengwa kwa kanuni rahisi, kila klabu hufanya kazi kwa uhuru na kwa kufuata sheria.”

Taarifa hiyo imetolewa kufautai malalamiko ya Ronaldo kuhusu klabu yake ya Al Nassr kushindwa kufanya uhamisho wakati wa dirisha dogo la Januari 2026.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 41, tayari amekosa mechi moja ya ligi na inasemekana, huenda akakosa mechi nyingine leo Ijumaa, Februari 6 dhidi ya Al-Ittihad kutokana na kutoridhishwa na usimamizi wa klabu.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: