Nahodha wa zamani wa klabu ya Barcelona Lionel Messi ametembelea uwanja mpya wa Barcelona kwa siri Usiku wa kuamkia leo
Messi
"Jana usiku nilirudi sehemu ambayo ninaikumbuka sana. Mahali ambapo nilikuwa na furaha sana, ambapo ulinifanya nijisikie mara elfu ya mtu mwenye furaha zaidi duniani. Natumai siku moja nitarudi, na sio tu kusema kwaheri kama mchezaji, kwani sikuweza kufanya".
Siku kadhaa zilizopita rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta alizungumza kuwa anahitaji kumuona tena Lionel Messi akitembelea Barcelona na kutoa heshima katika uwanja wao mpya New Sportify Camp Nou
Chanzo; Bongo 5