Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Gamond Apewa Miaka Miwili Stars

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imemtangaza rasmi Miguel Gamond kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Paul Makonda, amesema Gamond amepewa mkabata huo baada ya serikali kuridhishwa na kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi kifupi alichokuwa amekabidhiwa timu hiyo.

"Serikali imeamua kumpa Gamond jukumu la kuionoa timu yetu ya Taifa kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha muda mfupi alipokuwa amekabidhiwa timu hiyo," amesema Makonda.

Amesema kocha huyo amekuwa miongoni mwa makocha bora ambao anaamini kupitia uwezo wake dunia nzima itaitambua Tanzania.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: