Kwa mujibu wa ripoti ya FotoMac, mtandao unaojipambanua wenyewe kuwa ni namba moja kwa michezo huko Uturuki, ukiwa na wafuasi kibao kwenye mitandao ya kijamii, imebainisha Galatasaray imeanza mchakato wa kumvuta Lionel Messi akakipige Istanbul.
Na ripoti hiyo imetolewa na mhariri mkuu, Zeki Uzundurukan, ambaye amesema Messi, 38, anafuatiliwa kwa karibu sana na mabosi wa Galatasaray.
Imeelezwa kwamba Messi anaweza kukubali ofa ya mkopo wa miezi minne kwa sababu anataka kujiweka fiti katika kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026.
Messi kwa sasa anavuta Pauni 15 milioni kwa mwaka huko Miami, huku mshahara wake ukilipwa na Adidas na Apple. Galatasaray ipo tayari kulipa sehemu ya mshahara huo endapo kama atakubali kwenda kujiunga na kikosi chao kwa kipindi hicho cha miezi minne.
Chanzo; Mwanaspoti