Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Don Jazzy Ahaidi Milioni 250 Kila Mchezaji Super Egles

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, Don Jazzy, ameahadi kumzawadia kila mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) kiasi cha dola za Marekani 100,000 (Sh250 milioni) endapo wataweza kuifunga Morocco na kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Kauli hiyo imekuja wakati Super Eagles ikijiandaa kwa mechi hiyo muhimu itakayopigwa baadae leo Jumatano, Januari 14, huku mashabiki wa Nigeria wakijawa na hamu na matumaini makubwa ya kuona timu yao ikipata mafanikio makubwa katika mashindano hayo.

Don Jazzy amesisitiza kuwa anawapigia debe wachezaji na kuamini kuwa watafanikiwa kufikia lengo hilo kubwa, huku akiwahamasisha Super Eagles kuendelea kuonyesha uwezo wao wa hali ya juu uwanjani.

Mashabiki wa Nigeria wanajivunia ahadi hiyo, ambayo wanaamini ni motisha kwa wachezaji wa Super Eagles, ambao wanatakiwa kupambana kwa dakika zote 90 na kupata matokeo chanya.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: