Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

WiFi 8 Inayoweza Kuunganishwa na AI Kuanza Kutumika Mwaka Huu

Teknolojia mpya ya WiFi 8 (IEEE 802.11bn) imeanza kuvutia ulimwengu wa teknolojia baada ya kutambulishwa rasmi kwenye mkutano wa CES 2026. Kwa mujibu wa watengenezaji na wataalamu wa mitandao, teknolojia hii inatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia mwaka huu 2026 hadi 2028, kupitia vifaa mbalimbali vya kisasa.

Tofauti kuu ya WiFi 8 ni uwezo wake wa kuunganishwa na teknolojia ya AI, ambayo inafanya mtandao kutoa intaneti yenye kasi na utulivu wa hali ya juu. AI itasaidia kuboresha namna data inavyosambazwa, kupunguza ucheleweshaji (latency) na kuongeza ufanisi wa mtandao hata katika maeneo yenye vifaa vingi vinavyotumia intaneti.

Hii ni habari njema kwa watumiaji wa nyumbani na biashara, kwani WiFi 8 italeta mabadiliko makubwa katika matumizi ya intaneti, hasa kwa huduma za streaming, gaming na vifaa vya smart home.

Inatarajiwa kuwa mwanzo wa enzi mpya ya mtandao wa kisasa, wenye uwezo mkubwa na wa haraka zaidi kuliko teknolojia zilizopita.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: