Watumiaji wa WhatsApp wanaotumia mfumo wa iOS wanatarajiwa kunufaika na maboresho mapya yatakayorahisisha uwepo wa nafasi kwenye simu zao.
Kwa mujibu wa taarifa, mfumo huo mpya utawezesha watumiaji kusafisha kwa urahisi chati, video, picha na nyaraka mbalimbali zinazochukua nafasi kubwa kwenye simu.
Watumiaji wa iPhone sasa wataweza kuchagua aina tofauti za media files moja kwa moja kupitia WhatsApp na kuona kiwango cha storage kilichotumika baada ya kupakua audio, video au documents.
Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi na kuwapa watumiaji udhibiti zaidi wa nafasi ya simu zao kwa urahisi na haraka.
Chanzo; Mwananchi Scoop