Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Jinsi ya Kuchagua Benki Bora kwa Usalama wa Pesa Zako

Ulimwengu huu wa sasa na karne hii ya 21 na zijazo, Hakuna kitu kinamfanya binadamu wa kidijitali awe na faraja na kujihisi mwenye usalama wa kutosha ikiwa kiasi cha fedha anachomiliki kitakuwa salama.

Tupilia mbali nyakati teknolojia haijakuwa tuzungumzie kipindi hiki ambacho usalama wa pesa umehamia kidigitali zaidi, hapa kuba njia kadhaa zitakazo kusaidi kuchagua benki bora kwa usalama wa fedha zako, Hii kwa wewe uliye Tanzania, Kenya, Uganda.

1. Hakikisha benki ina leseni rasmi kutoka Benki Kuu:  
- Kenya: CBK  
- Tanzania: BoT  
- Uganda: BoU  
Angalia orodha rasmi kwenye tovuti yao. Epuka "benki" zisizo na leseni au zinazotangaza sana bila uthibitisho.

2. Angalia ulinzi wa amana (deposit insurance) – hii ndiyo kinga ya kwanza ikiwa benki itaanguka:  
- Kenya (KDIC): hadi KSh 500,000 kwa kila mteja kwa benki moja (hadi Juni 2026).  
- Tanzania (DIB): hadi TZS 7.5 milioni kwa kila mteja (imeongezeka hivi karibuni).  
- Uganda (DPF): hadi UGX 10 milioni kwa kila mteja.

Ikiwa una pesa zaidi ya kiwango hicho, Usiweke, benki moja Gawanya katika benki 2 au 3 kila moja italinda kiasi chake tofauti. Hii inaongeza ulinzi wako.


3. Chagua benki kubwa na imara zenye historia ndefu na mtaji mkubwa (hatari ndogo ya kuanguka)


•Kenya: KCB, Equity, Co-op Bank, NCBA, Stanbic, Absa, Standard Chartered, I&M.  

•Tanzania: CRDB, NMB, NBC, Exim, Absa, Standard Chartered, Azania, TPB.  

•Uganda: Stanbic, Centenary, Equity, dfcu, Absa, Standard Chartered.  
Hizi zina mtandao mkubwa, faida thabiti na ripoti chache za matatizo makubwa.


4. Zingatia usalama wa kidijitali:  
- App/internet banking iwe na 2FA, OTP, alama ya kidole au uso).  
- Iwe na alerts za SMS/email kwa kila shughuli.  
- Hakuna ripoti nyingi za udukuzi au matatizo kwenye habari.

Mambo ya Kuzingatia:  
- Gawanya pesa (diversify).  
- Akaunti tofauti: moja ya kila siku (kidogo), akaunti ya akiba (nyingi).  
- Pesa kubwa sana? Fikiria treasury bills au money market funds za serikali.  
- Angalia taarifa zako kila siku.  

Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: