Kampuni ya Adobe imeanzisha mfumo mpya unaowawezesha watumiaji wa ChatGPT kuhariri picha na nyaraka moja kwa moja kupitia jukwaa hilo. Kupitia ushirikiano huu, watumiaji sasa wanaweza kutumia programu maarufu za Adobe kama Photoshop, Acrobat na Adobe Express bila kulazimika kufungua programu hizo.
Mfumo huu unawapa watumiaji uwezo wa kuunda na kuhariri (edit) picha, kuboresha mwonekano wa picha (kama vile ku-blur background), pamoja na kurekebisha mafaili ya PDF kwa urahisi. Kinachovutia zaidi ni kuwa huduma hii inapatikana bure kwa watumiaji wa ChatGPT.

Ili kutumia huduma hii, mtumiaji anahitaji kufungua programu ya ChatGPT na kuandika ombi lake moja kwa moja, kwa mfano: “Adobe Photoshop, help me to blur the background of this image.” Baada ya hapo, ataambatanisha picha husika.
Kwa mfumo huu mpya, kazi za uhariri sasa zinafanyika haraka na kwa ufanisi, sawa na kutumia programu yenyewe ya Adobe Photoshop.
Chanzo; Mwananchi