Kampuni ya Apple imepata hasara kubwa baada ya uzinduzi wa iPhone 17, ambapo hisa zake zilipungua kwa 1.5% na kushuka hadi 612,285/= tsh kwa hisa moja hali iliyofanya kampuni hiyo kupoteza zaidi ya dola bilioni 112 sawa na 305.76 trilioni za kitanzania katika thamani ya soko.
Ripoti za media zinasema hasara hiyo imetokana na mauzo ya chini ya iPhone 17. Simu hiyo iliyopewa hadhi ya juu ina kamera yenye viwango vya juu, rangi za bold na black, pia ni nyembamba zaidi, lakini bado haijapata mafanikio makubwa.
Zaidi, bei ya hisa za Apple zimepolomoka hadi 612,285/= kutoka 620,232/= baada ya uzinduzi wa iPhone 17.
Chanzo: Tanzania Journal