Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Gari ya Rais wa Marekani Linavyotengenezwa

Katika ulimwengu wa magari ya kifahari, hakuna gari linalozua heshima, mshangao, na hofu kama limousine ya Rais wa Marekani, maarufu kama The Beast.

Hili si gari la kawaida. Ni ngome inayotembea, iliyojengwa kwa siri na chini ya ulinzi mkali, kwa lengo moja kuu: kumlinda rais wan chi kubwa duniani kwa gharama yoyote ile.

Leo, tunaingia ndani ya simulizi ya siri ya jinsi The Beast anavyotengenezwa—kuanzia kiwandani hadi barabarani.

Ingawa lina nembo ya Cadillac, The Beast si gari la kawaida la kifahari.

Hutengenezwa na General Motors chini ya uangalizi mkali wa Idara ya Ulinzi wa Rais, U.S. Secret Service.

Tofauti na magari ya kawaida, The Beast hujengwa juu ya chasis ya lori nzito, iliyoundwa kubeba uzito mkubwa wa silaha, kinga, na teknolojia za kisasa za kiusalama.

Uzito wake unakadiriwa kufikia tani tisa.

Utengenezaji wa The Beast huanza kwa kanuni moja muhimu, ulinzi kwanza.

Milango yake ina unene wa karibu sentimita ishirini, ikiwa na uzito unaokaribia mlango wa ndege.

Madirisha yake yametengenezwa kwa tabaka nyingi za kioo kisichopenyeka risasi.

Ni dirisha moja tu la dereva linaloweza kushushwa, na hata hilo, kwa sentimita chache sana.

Ndani ya mwili wa gari, mafundi huweka paneli za kinga zilizotengenezwa kwa chuma, titanium, na kauri, vifaa vinavyotumika kwenye magari ya kivita ya kijeshi.

Chini ya mwonekano wake wa kifahari, The Beast limejaa mifumo ya siri.

Tangi la mafuta limefungwa kwa povu maalum la kuzuia milipuko.

Matairi yake ya Kevlar hayawezi kupasuka, na hata yakipigwa risasi, gari linaweza kuendelea kukimbia.

Mfumo wa breki umeimarishwa kuhimili uzito mkubwa hata kwenye hali za dharura.

Zaidi ya hapo, kabati la rais linaweza kufungwa kabisa na kujitegemea kwa hewa safi, kuzuia mashambulizi ya kemikali au kibiolojia.

The Beast si usafiri tu, ni kituo cha amri kinachosafiri.

Ndani yake kuna mifumo ya mawasiliano ya siri, inayomwezesha rais kuwasiliana na jeshi, serikali, na vyombo vya usalama popote alipo duniani.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: