Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mercedes Benz Kuanza Kutumia Engine ya BMW 2027

Kampuni ya magari ya kifahari Mercedes-Benz inaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya hatua ya juu ya makubaliano ya kutumia injini kutoka kwa mpinzani wake wa muda mrefu, BMW.

Kwa mujibu wa taarifa, mpango huo unaeleza kuwa kuanzia mwaka 2027, Mercedes-Benz itanunua injini za petroli za silinda nne (2.0L turbo) kutoka BMW.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na shinikizo la gharama, mahitaji ya teknolojia ya magari ya mseto (plug-in hybrid) pamoja na changamoto zinazoikabili kampuni hiyo katika maendeleo ya injini zake mpya.

BMW inatarajiwa kusambaza injini yake iliyothibitishwa ya 2.0L turbo hatua itakayosaidia Mercedes kupanua safu ya magari yake ya hybrid huku ikipunguza gharama za utafiti na maendeleo.

Kwa upande wa BMW makubaliano hayo yataongeza uzalishaji na mapato.

Wengi wanautaja kama uamuzi wa busara wa kibiashara kwa ajili ya kuhimili ushindani, huku wengine wakiona ni pigo kwa fahari na utambulisho wa chapa ya Mercedes-Benz katika soko la magari ya kifahari.

 

 

Chanzo;  Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: