China imeingia katika hatua mpya ya mapinduzi ya kiteknolojia kwa kuanzisha matumizi ya magari ya kusafirisha mizigo bila dereva, maarufu kama robovans, yanayoendeshwa kwa kutumia mfumo wa akili mnemba.
Lengo kuu la ubunifu huo ni kupunguza gharama za uendeshaji, kuongeza ufanisi na kutoa huduma za usafirishaji zinazofanya kazi saa 24 bila kusimama.
Hata hivyo, pamoja na matumaini hayo makubwa, matumizi ya magari haya katika miji yenye msongamano na mazingira yasiyotabirika yamezua mjadala mpana.
Chanzo; Dw