Indonesia imekuwa nchi ya kwanza duniani kuzuia matumizi ya chatbot ya Grok, inayomilikiwa na bilionea Elon Musk, kufuatia wasiwasi mkubwa kuhusu usambazaji wa picha na maudhui ya ngono ya kubuniwa kwa kutumia Akili Mnemba (AI).
Waziri wa Mawasiliano na Masuala ya Kidijitali wa Indonesia amesema kuwa matumizi ya deepfake za kingono bila ridhaa ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, utu wa mtu, na usalama wa raia katika mazingira ya kidijitali.
Serikali imeeleza kuwa teknolojia hiyo imekuwa ikitumiwa kutengeneza picha za uongo zinazoathiri hasa wanawake na watoto.
Hatua hiyo imezua mjadala wa kimataifa kuhusu mipaka ya matumizi ya AI, uwajibikaji wa kampuni za teknolojia, na jukumu la serikali kulinda raia dhidi ya madhara ya teknolojia mpya.
Chanzo; Cnn