Wafanyabiashara wa biashara ndogondogo wote waliopanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara za kuingia soko la Kariakoo wametakiwa kuondoa bidhaa zao na kuziacha baarabara hizo wazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ameyasema hayo leo February 6 mbele ya Waandishi wa Habari na kusisitiza kwamba wote waliopanga bidhaa zao pembenni ya barabara wanasababisha kuzifunga barabara za soko hilo.
Ameongeza kuwa kuondoka katika sehemu hizo kutasaidia kuziacha barabara wazi na kurahisisha shughuli za kibiashara kutokana na soko hilo kuwa na mwingiliano mkubwa wa Watu kutoka ndani na nje ya Nchi.
Chanzo; Millard Ayo