Mamlaka ya Kitaifa ya Viwango nchini Uganda (UNBS) imetoa tahadhari, ikisema kuwa zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zinazouzwa sokoni nchini humo ni feki au hazikidhi viwango vinavyokubalika.
Kwa mujibu wa UNBS, hali hiyo inatishia afya ya wananchi, usalama wa watumiaji na inavuruga ushindani wa haki katika soko. Bidhaa hizo feki zinatajwa kujumuisha vifaa vya elektroniki, vipodozi, dawa, vyakula, pamoja na bidhaa za ujenzi.
Mamlaka hiyo imeeleza kuwa imeongeza juhudi za kudhibiti hali hiyo kwa kufanya ukaguzi wa kina, kuelimisha umma na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanyibiashara walaghai.
Chanzo: Dw