Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

CEO Roundtable of Tanzania Yatimiza Miaka 25

Jukwaa la Wakurugenzi Wakuu wa Tanzania (CEO Roundtable of Tanzania – CEOrt) linaadhimisha miaka 25 ya uongozi endelevu wa sekta binafsi nchini, likijivunia mchango wake katika safari ya mageuzi ya kiuchumi, kuimarisha uongozi katika sekta binafsi na umma, pamoja na kukuza mashauriano na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali katika nyanja mbalimbali za kisera na kiuchumi.
 

Mjumbe wa Bodi ya CEOrt na Mkurugenzi wa Rex Corporate, Dkt.Alex Nguluma wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, Mabalozi, watalaam na watu mashuhuri wanategemea kuhudhuria maadhimisho hayo kama wadau muhimu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “Urithi Unaoendelea Kusonga” (Legacy in Motion) yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Januari 31, 2025 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CEOrt, Bw. David Tarimo, amesema jukwaa hilo linalojumuisha wanachama 238 kutoka makampuni mbalimbali limekuwa na mchango mkubwa katika kuchochea uwekezaji wenye tija, kutoa ajira kwa Watanzania, na kuchangia mapato ya kodi kwa maendeleo ya taifa.

Bw. Tarimo amesema CEOrt ilianzishwa mwaka 2000 katika kipindi muhimu cha mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania, wakati kulipojitokeza hitaji la kuwepo kwa jukwaa la kuaminika la kuwaunganisha viongozi wakuu wa sekta binafsi, umma ,watunga sera na watendaji  serikalini.

Ameeleza kuwa moja ya mafanikio ya awali ya CEOrt ilikuwa ni ushiriki wa ngazi ya juu ulioanzishwa chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa, ulioweka msingi wa dhana kwamba maendeleo endelevu hupatikana kwa nguvu zaidi pale serikali na sekta binafsi zinaposhirikiana kupitia majadiliano ya wazi, yaliyopangwa na yenye kuaminiana.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Bi. Santina Benson, amesema kuwa kati ya mwaka 2005 na 2010, jukwaa hilo liliimarisha zaidi mchango wake kwa kuwekeza katika uongozi na uimarishaji wa taasisi. 

Kipindi hicho kilishuhudia kuanzishwa kwa mipango mbalimbali ikiwemo Mfuko wa ufadhilk wa masomo wa Wakurugenzi Wakuu (CEO Scholarship Fund), Mpango wa Kuimarisha Uongozi katika Utumishi wa Umma (Enhancing Public Service Leadership – EPSL), pamoja na Kikosi Kazi cha 3PF ambacho kiliunga mkono juhudi za mageuzi katika sekta ya umma, ikiwemo Mpango wa Mageuzi ya Jeshi la Polisi.

Bi. Santina amesema kuwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, CEOrt ilijitambulisha zaidi kama jukwaa la majadiliano kuhusu utawala bora na uwajibikaji.

Pia Kati ya mwaka 2015 na 2020, taasisi hiyo iliweka rasmi ajenda ya Biashara na Uendelevu kupitia ushirikiano na taasisi mbalimbali zikiwemo Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN).

Katika kipindi hicho, CEOrt pia ilizindua programu ya Mpango wa mafunzo kwa viongozi kutoka makampuni mbalimbali ijulikanayo kama CEO Apprenticeship Programme (CAP), iliyolenga kuandaa viongozi wa baadaye wa sekta binafsi na umma, ambapo Watanzania wengi wamefanikiwa kushika nafasi za uongozi wa juu katika taasisi na makampuni mbalimbali nchini toka mpango huu uanzishwe.

Katika awamu ya hivi karibuni (2020–2025), CEOrt imeimarisha mkazo wake katika ukuaji shirikishi, uongozi wa maadili, na ustahimilivu wa muda mrefu.

 Mipango kinara kama Think Equal, Lead Smart (TELS) imeanzishwa kwa lengo la kusaidia biashara zinazoongozwa na wanawake hapa nchini ili kuwajengea uwezo.

Kuhusiana na mada hii: