Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Arusha wametoa tamko la kutaka kufunga maduka yao kwa kile walidai Wamachinga kuvamia barabara na kufanya biashara mbele ya maduka yao kitendo kinachopekea wao kutokufanya biashara inavyostahili licha ya kuwa wanalipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Akizungumza na Wanahabari Mwenyekiti wa Wafanya Bishara Mkoa wa Arusha Lonken Massawe amesema licha ya wamachinga kupangiwa maeneo yao ya kwenda kufanya biashara lakini wamegoma kwenda
“Ndugu waandishi nimewaita leo kuzungumza na nyie kuhusu kadhia inayotukumba ya wamachinga na kwa kifupi hata nyinyi wenyewe mnaona tumeingiliwa na wamachinga na wenye maduka sasa wako tayari kufunga maduka yao kwa sababu wanasema wamachinga wamechukua sehemu ile ya biashara ambayo wao wanailipia kodi na wamesema kipindi hichi ndio cha kulipa kodi za serikali lakini kipindi kimekuwa kigumu sana kwa sababu hawana nafasi ya kuuza kile walicho nacho.” Amesema Mwenyekiti wa Wafanya Biashara mkoa wa Arusha.
Aidha kwa upende wake Kaimu Mkurugenzi jiji la Arusha amesema kuwa swala hilo halijafikishwa katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji na amewataka walalamikaji kuweza kufika Ofisini kwake ili waweze kuketi na kuzungumza jinsi watakavyoweza kutatua changamoto hiyo.
Chanzo; Millard Ayo