Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tanzania, Uganda Zakubaliana Kuondoa Vikwazo vya Kibiashara

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni leo February 07,2026 pamoja na mambo mengine wameongelea kuhusu kuondosha vikwazo vya kibiashara kati ya Tanzania na Uganda ili kukuza uchumi wa Nchi hizi mbili.

Akiongea Ikulu ya Dar es salaam leo, Rais Samia amesema “Tumeongea kuhusu kuondosha vikwazo vya biashara tumekuwa tukiongea mara nyingi vikwazo hivi kila tukiviondoa biashara zinakua, biashara zimekua ndani ya Afrika Mashariki lakini kuna vikwazo ambavyo Watendaji na Watu wetu wanaviweka ila tumezungumza kuviondosha ili kutengeneza soko zuri la Afrika Mashariki”

“Timu zetu za Mawaziri na Wasaidizi wao walikuwa wana mazungumzo waendeje kuyamaliza, la kwanza kuhusu ujenzi wa mabomba ya nishati ikiwemo la kuchukua mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga Bandarini na tunamshukuru huenda kuanzia mwezi July mwaka huu huenda meli ya kwanza ikaondoka Tanga kwenda yanakopelekewa, la pili kama mnavyojua sasa hivi Nchi zetu ambazo hazina Bahari wanategemea Bandari zetu za Dar na Tanga tumezungumza jinsi watakavyopata nafasi ya kutumia Bandari hizi”

 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: