Zambia imeandika historia kwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kukubali sarafu ya China (yuan) katika ulipaji wa kodi za sekta ya madini. Hatua hii inaonyesha kuongezeka kwa ushawishi wa kifedha wa China katika rasilimali muhimu za Afrika, hususan shaba.
Benki Kuu ya Zambia imesema uamuzi huo unalenga kurahisisha usimamizi wa akiba ya fedha za kigeni na kupunguza gharama za kulipa madeni ya China, ambayo ni mshirika mkubwa wa biashara ya shaba na mkopeshaji wa Zambia.
Hatua hii inaonekana kama mabadiliko ya kimkakati katika mfumo wa kifedha wa Afrika, huku baadhi ya wachambuzi wakiona ni ishara ya kupungua kwa utegemezi wa dola ya Marekani.
Chanzo; Cnn