Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Machinga Kuondolewa Barabarani Kariakoo, Soko Kuongezewa Thamani

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kuchukua hatua ya kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyo rasmi.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo.

“Inawezekana lisiwe jambo zuri na yanaweza kuwa maelekezo machungu kwa wafanyabiashara, lakini huwezi kujenga nyumba yenye thamani ukaziba barabara. Naamini diplomasia itaendelea kutumika pasipo kutumia nguvu kwamba barabara zitabaki wazi,” amesema RC.

Akizungumza katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chalamila amesema kuanza kwa huduma katika Soko Kuu la Kariakoo kutaambatana na kufunguliwa kwa barabara zote zinazoingia na kutoka sokoni humo.

Februari 17, 2026 Jana, Jumanne , katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo, kulikuwa kumebandikwa matangazo yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, akiwataka wafanyabiashara wanaopanga na kuuza bidhaa katikati ya barabara za mitaa na njia za waenda kwa miguu ambao hawajapangwa waondoe bidhaa zao mara moja.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: