Kufungua swaumu ni hatua muhimu baada ya saa nyingi za kujinyima chakula na kinywaji.
Ni wakati ambao mwili unahitaji kurejeshewa nguvu, maji na virutubisho vilivyopungua kwa muda wa mchana.
Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanaonya kuwa si kila chakula kinafaa kuliwa mara tu baada ya kufuturu, kwani baadhi vinaweza kusababisha uchovu, kujaa kwa tumbo au hata kudhoofisha afya.
Baada ya muda mrefu bila kula, mfumo wa mmeng’enyo huwa katika hali ya utulivu na hufanya kazi polepole. Kuingiza vyakula vizito ghafla kunaweza kuushtua mwili na kuleta usumbufu.
Miongoni mwa vyakula vinavyoshauriwa kuepukwa wakati wa kufungua ni vile vyenye mafuta mengi. Vyakula vya kukaanga kama sambusa, bhajia, vitumbua na chipsi, kwani huongeza mzigo kwa tumbo na kusababisha kichefuchefu, uchovu na tumbo kujaa haraka.
Mbali na hilo, mafuta mengi huongeza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa.
Chanzo; Mwananchi