Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Nguo Fupi Marufuku Zanzibar Kipindi cha Ramadhani

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imewataka Watalii, Wafanyabiashara na Wadau wa utalii Zanzibar kuheshimu maadili ya Dini na Utamaduni uliopo Zanzibar kipindi hiki cha kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kamisheni imesema ni lazima Migahawa na sehemu za chakula zilizo nje ya Hoteli zifungwe hadi wakati wa jua kuzama (IFTAR) na kupiga marufuku kula, kunywa au kuvuta Sigara hadharani wakati wa mchana na kusisitiza Watu wakiwemo Wageni kuvaa mavazi yenye staha katika maeneo ya Umma.

Kamisheni hiyo imepiga marufuku uvaaji wa mavazi yanayoonesha sehemu za mwili na kuwataka Wadau wa Utalii Visiwani humo kuwakumbusha Wafanyakazi juu ya muongozo huo na kubandika matangazo pale inapobidi.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: