Uchunguzi wa kisayansi umeonyesha kuwa kukaa kwa muda mrefu kwa siku kunaweza kukuua.
Ulimwengu tunaoishi sasa sio mkubwa kama ilivyokuwa zamani. Zamani watu walikuwa wakitembea, kwenda sokoni, kulima, kuwinda, na kusafiri.
Ulimwengu wa kisasa unahimiza kukaa kwa muda mrefu, iwe watu wanataka au la. Watu wengi hutumia saa nyingi wakiwa wameketi (kukaa) kwenye gari, shuleni, ofisini, nyumbani hasa tunapotazama TV.
Wanasayansi na wataalamu wa matibabu wameonyesha kuwa kukaa kwa muda mrefu kunaweza kusababisha hali nyingi mbaya za afya ambazo zinaweza kukudhoofisha.
Baadhi ya magonjwa na hali ya kiafya ambayo kukaa kwa muda mrefu kunaweza kusababisha ni pamoja na: Kisukari, magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, unene (unaosababisha magonjwa mengine mengi) na kifo.
Mtaalamu mmoja nchini Uingereza, Dk Emma Wilmot alithibitisha hilo huku akieleza kuwa utafiti wao ulionyesha kuwa watu wanaokaa chini kwa muda mrefu mara nyingi hupata magonjwa hayo.
Ukweli ni kwamba imefanyiwa utafiti kuwa kukaa muda mrefu huathiri utengenezwaji wa nishati katika mwili wa binadamu iitwayo ‘Glucose’ pamoja na kitu kiitwacho ‘insulini’ ambacho ndicho husaidia Glucose kuwa kwenye damu ya binadamu. Wakati mwingine watu hutumia saa nyingi wakiwa ndani ya gari.
Mtaalamu mwingine Dk.Udodi Okoli naye anasema “Kuketi kwa muda mrefu kunaweza kuleta matatizo kwenye mgongo wa mtu hasa mtu asipokaa vizuri au hutumia kiti kisichotengenezwa kwa ajili ya kukaa vizuri kwa muda mrefu.”
Alieleza kuwa mtu akikaa kwa muda mrefu mbele ya kompyuta yake na asiweke kichwa au shingo yake kwa njia ifaayo, shingo inaweza kuanza kuwa na maumivu.
Chanzo; Global Publishers