Licha ya kuonekana ni ishara ya werevu, taaluma na unadhifu lakini imeelezwa kuvaa tai kunaweza kupunguza mtiririko wa damu kwenye ubongo kwa asilimia 7.5.
Utafiti uliofanywa mwaka wa 2018 uligundua kuwa kuvaa tai iliyobanwa sana kunaweza kupunguza mtiririko wa damu kwenye ubongo wako kwa hadi asilimia 7.5, jambo ambalo linaweza kukufanya uhisi kizunguzungu.
Kwa mujibu wa BBC Science Focus mbali na kizunguzungu pia kichefuchefu na kusababisha maumivu ya kichwa.
Pia zinaweza kuongeza shinikizo machoni mwako ikiwa zimebana sana na zina uwezekano mkubwa wa kubeba vijidudu.
Chanzo; Mwananchi