Karne ya 10, askari wa farasi wa Uajemi walivaa viatu vyenye visigino ili kuzuia miguu isiteleze walipokuwa juu ya farasi vitani. Visigino hivyo vilisaidia mguu kukaa imara kwenye stirrup wakati wa mapambano.
Baadaye, mtindo huu uliingia barani Ulaya na kuanza kuhusishwa na utajiri na hadhi ya juu. Miongoni mwa walioufanya kuwa maarufu alikuwa Louis XIV wa Ufaransa, aliyependelea high heels zenye visigino vyekundu ili kuongeza kimo chake na kuonyesha mamlaka ya kifalme.
Katika kipindi hicho, mwanaume aliyekuwa akivaa high heels alionekana kama mtu wa tabaka la juu ishara kuwa hafanyi kazi ngumu za mikono, bali ni wa heshima na mamlaka.
Kwa kifupi: High heels zilianza kama silaha ya vita, zikageuka alama ya utajiri kabla hazijawa fasheni ya leo maarufu kwa Wanawake.
Chanzo; Global ublishers