Usipige Makelele
Kumbuka sio wewe tu unaeenda kutembelea misitu hivyo jiepushe na vitendo ambavyo vitakuwa kero kwa watumiaji wengine wanaoenda kwa lengo la kufurahia uoto wa asili na kutafuta utulivu wa akili toka makelele ya mijini. Epuka kusikiliza muziki kwa sauti kubwa au kupiga kelele.
Ondoka na kumbukumbu tu
Kitu chochote ulichokikuta msituni usikibebe na kuondoka nacho, waachie wengine wakija wakione. Hata hivyo hujazuiwa kupiga picha na kupata kumbukumbu.
Usiwe chanzo cha moto
Katika msimu wa kiangazi kumekuwa na matukio ya misitu kuteketea kwa moto. Ili kuepusha hili kutokea unashauriwa kuhakikisha unavuta sigara katika maeneo ambayo hakuna miti au majani makavu. Inapotokea umeweka kambi na unalazimika kuwasha moto au kujipikia, chukua tahadhari moto usihame kwenye majani.
Jali na heshimu watu wengine
Watu tofauti wanatembelea misitu na wangependa kufurahia mandhari kama wewe, hivyo jitahidi kuwajali watu wengine kwa kutoharibu wakati mzuri wanaopitia.